MUFTI MKUU BW,ISSA SHABANI SIMBA,NI MMOJA KATI YA WALIOPINGA VIKALI KITENDO HICHO,HASA KABLA MWEZI HUU WA RAMADHAN KABLA HAUJAANZA,ALISISITIZA WOTE WALIO KATIKA MAHUSIANO YA UCHUMBA WAWEZE KUKAMILISHA NDOA ZAO KABLA YA KUINGIA KWENYE MFUNGO KWANI KWAKUWA KINYUME NA HILO NI DHAMBI NA WALA SI SWAWABU KWA KILA MUHUSIKA.
.
MAALIM HASSAN YAHAYA,NAYE NI MMOJA KATI YA VIONGOZI WENYE HESHIMA KUBWA KWA UISLAM NCHINI WALIOCHUKIZWA NA KITENDO CHA MSANII DIAMOND,AMEDAI SI VYEMA KUFUTURU NA KIMADA NA HATA PIA SI SAHIHI MWANAMUME KUANDALIWA FUTARI NA KIMADA,KWA KUFANYA HIVYO NI DHAMBI NA WALA SI SWAWABU HATA KAMA UNAFUNGA MPAKA SITA.
SHEIKH ALHADI MUSSA,SHEIKH MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM,PIA NI MMOJA KATI YA WALIOLIONGELEA HILI KWA MTAZAMO SAWA NA MASHEIKH WENZIWE.
SHEIKH KHAMIS MATAKA,KATIBU MKUU WA TAASISI YA MASHEIKH NA ANAZUONI NCHINI,AMESEMA LENGO LA SWAUMU NI KUMFANYA MTU KUWA MCHAMUNGU,NA MCHAMUNGU NI YULE ANAYEFUATA YOTE YANAYOAMRIWA NA MWENYEZI MUNGU YAFUATWE,NA KUACHA YOTE ALIYOYAKATAZA,SASA KUWA NA HAWARA HAIKUBALIKI,NA WALA SI KWA KIPINDI HIKI CHA RAMADHAN BALI KWA KIPINDI CHOTE HATA NJE YA MWEZI HUU WA MFUNGO,SASA SWALA LA KUFUTURU NA KIMADA NI DHAMBI.
JUMUIYA YA KIISLAM NCHINI,IKIONGOZWA NA BAADHI YA VIONGOZI WAKUBWA KATIKA DINI HIYO NCHINI,AKIWEMO MUFTI MKUU SIMBA,WAMELAANI VIKALI KITENDO CHA MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA NCHINI DIAMOND KUFUTURU PAMOJA NA KIMADA WAKE BIBIE PENIELI MANGILWA.
No comments:
Post a Comment