Tuesday, 25 February 2014

Baraza la mawaziri lajiuzulu Misri

Waziri mkuu wa Misri, Hazem el-Beblawi na baraza lake la mawaziri wamejiuzulu.
Katika taarifa ya moja kwa moja kupitia televisheni, Bwana El-Beblawi alisema kuwa Misri imeshuhudia ongezeko la migomo katika sekta ya umma katika wiki chache zilizopita.
Alisema kuwa hakuna hata serikali moja duniani ambayo inaweza kutimiza mahitaji ya watu wake katika kipindi kifupi sana.
Serikali hiyo ya mpito ilianza kazi mwezi Julai mwaka jana baada ya jeshi kumpindua aliyekuwa Rais Mohammed Mosri
Taarifa zinasema kuwa uamuzi wa baraza la mawaziri kujiuulu ulitokea baada ya mkutano kati ya mkuu wa majeshi na waziri wa ulinzi Field Marshal Abdul Fattah al-Sisi.
Inaarifiwa kuwa al-Sisi anatarajiwa kujiuzulu kutoka katika wadhifa wake ili kugombea Urais.
SOURCE:BBC SWAHILI.

No comments: