John Kerry |
Marekani haikufurahishwa na hatua ya Uganda kuidhinisha sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.
Waziri wa mashauri ya Kigeni wa Marekani,Bw John
Kerry amesema tangu Uganda iidhinishe mswada huo miaka minne iliyopita,
Marekani ilieleza wazi kwamba sheria hiyo inakiuka jukumu la kuhakikisha
kuwepo haki za binaadamu ambalo tume ya haki za binaadamu Uganda
inatambua linaambatana na sheria ya Uganda.Kerry amesema,' Baada ya kuidhinishwa sheria hii, tunaanza ukaguzi wa ndani wa uhusiano wetu na serikali ya Uganda, kuhakikisha kwamba pande zote za uhusiano wetu, ukiwemo miradi ya msaada, zinapinga sera na sheria zinazowaonea watu na tuwe na uhusiano unaodhihirisha maadili yetu'
Tamko hilo limetolewa siku moja baada ya rais Yoweri Museveni kukaidi shinikizo la kimataifa na kutia saini sheria hiyo iliyo zusha mzozo, inayoharamisha mapenzi ya jinsia moja Uganda, hatua iliyozusha hisia kali.
Baadhi ya mataifa ya magharibi tayari yanatishia kukatiza msaada wa moja kwa moja kwa serikali ya Uganda.
Marekani inasema kuidhinishwa kwa sheria hiyo kunatishia hatari ya kurudi nyuma katika uwajibikaji wa Uganda kulinda haki za raia wake na kutishia jamii ya wapenzi wa jinsia moja Uganda.
No comments:
Post a Comment