Kampuni ya mtandao wa Kijamii ya Facebook imesema
kuwa itaununua mtandao wa mawasiliano ya ujumbe mfupi wa WhatsApp kwa
kima cha dola bilioni kumi na sita, na nyongeza zaidi ya dola bilioni
tatu zitakazolipwa waanzilishi wa mtandao huo pamoja na wafanyikazi
wake.
Hiyo ndiyo biashara kubwa zaidi ya ununuzi kuwahi kutekelezwa na Facebook hadi kufikia sasa.WhatsApp ni maarufu sana miongoni mwa vijana wanaotafuta kuepuka kulipia huduma ya kutuma ujumbe mfupi wa simu yaani SMS.
WhatsAp imeweza kuwasajili zaidi ya watumiaji milioni mia nne hamsini.
Mark Zuckerberg |
Katika taarifa, mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg amesema kuwa mtandao huo upo njiani kuwaunganisha watu bilioni moja jambo litafanya Facebook kuwa na thamani kubwa.
SOURCE:-BBC SWAHILI.
No comments:
Post a Comment