Wednesday, 19 February 2014

NI VIGUMU KUIDHIBITI ARSENAL NDANI YA DAKIKA TISINI"PEP GUARDIOLA"KOCHA{BAYERN MUNICH}

Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola amekiri ni vigumu sana kudhibiti dakika tisini za mechi ya aina yeyote dhidi ya Arsenal ya Uingereza .
 Guardiola ambaye hajashinda katika mechi zake mbili uwanjani Emirates ,anatarajia ushindani mkalitoka kwa ARSENAL leo.
Licha ya hayo , Bayern Munich imeshindwa katika mechi mbili pekee msimu huu.
Bayern ilishindwa na Borussia Dortmund na Manchester City mapema katika mkondo wa kwanza wa ligi ya msimu huu.
Mwaka uliopita Bayern,iliilaza The Gunners 3-1 katika hatua hii ya Robo fainali.
Hata hivyo vijana wa Pep walifuzu kutokana na sheria ya bao la ugenini licha ya kushindwa 2-0 katika mkondo wa marudiano huko Ujerumani.

Guardiola

"Uunaweza cheza vizuri na utawale nyanja zote kwa dakika 30 ama 75 hivi lakini zile zitakazosalia utakabiliwa na upinzani mkali "
 Vijana wa Arsene Wenger hawajawahi kushinda taji lolote tangu mwaka wa 2005 lakini Guardiola anasisitiza kuwa sio timu hafifu kamwe.Ngoja tuone dakika tisini za mechi hii kali itakayochezwa leo ndani ya kiwanja cha EMIRATES STADIUM.

No comments: