Msanii BEN POL anatarajia kuachia movie yake ya kwanza mwezi huu, ni movie ambayo Ben Pol amemhirikisha mchekeshaji maarufu, Bi Kiroboto, movie hiyo iliyoandaliwa na kamupni ya Swahilihood itazinduliwa rasmi February 20 mwaka huu.
“Yaani mimi nimeienjoy sana, nilikuwa nafeel kama ni mama yangu mzazi”, alisema Ben Pol
Mratibu wa Swahilihood, Hassani Mrope ameiambia tovuti ya Times fm kuwa
filamu hiyo ya Sunshine itazinduliwa pamoja na filamu nyingine mbili
ambazo ni ‘Mdundiko’ na ‘Network’. Filamu hizo zitazinduliwa kuanzia saa
kumi na mbili jioni, Century Cinemax, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Huku Ben Pol akiongelea filamu hiyo kwa kumsifia muigizaji huyo wa kike
aliyecheza nae kama mama yake, Christina Mbunda maarufu kama Bi
Kiroboto.
Mwimbaji huyo alieleza kuwa mbali na kuigiza vizuri kama mama mwenye
moyo mzuri anayejali familia yake, hata katika uhalisia ni mama bora
anayejali.
“unajua bi Kiroboto, ukitoa upande wa kazi wa kuigiza, yaani ni mama
mmoja very humble. Yaani ni mama…anareal feeling ya mama …unajua hata
kama mko kwenye set kichwa kinauma au nini, yaani ana ile care ya mama.
Yaani mpaka nammiss.” Aliongeza Ben Pol.
Kwa mujibu wa Ben Pol, filamu hiyo ilishutiwa kwa muda wa mwezi mmoja.

No comments:
Post a Comment