![]() |
| magunia ya bangi |
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas, amedai kuwa Julai 25, 2014 kwamba tukio hilo lilitokea jana yake Julai 24, 2014 saa 20:30 usiku wakati Askari wa Jumuiya ya jamii wanaofanya ulinzi wa kulinda wanyamapori na mazingira katika Kambi ya Enduimet wakiwa doria waliona magunia hayo yakiwa yametelekezwa baada ya watuhumiwa kuhisi wanafuatiliwa.
“Watuhumiwa walipoona wanaweza kukamatwa waliamua kufungua magunia hayo ya bangi iliyokuwa imebebwa na wanyama aina ya Punda ambao mara nyingi huwatumia kusafirisha mizigo yao na kutokomea kusikojulikana,”
Alisema baada ya kupata taarifa za kuwepo watu wanaosafirisha bangi kupitia njia za ‘Panya’walianza kuwafatilia lakini hawakuweza kuwakamata kutoka na kubaini mtego huo na kuwa Jeshi hilo linaendelea kuwasaka watu hao.
Alifafanua kuwa watu hao walikua wakitokea maeneo ya Oldonyosambu wilaya ya Arumeru kuelekea Namanga katika mkoa huo na kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa wasafirishaji walikuwa wakielekea nchi jirani ya Kenya ambako inadaiwa kuwepo kwa soko la bidhaa hiyo iliyopigwa maarufuku hapa nchini.

No comments:
Post a Comment