Friday, 28 February 2014

Mtu mmoja afariki dunia, 38 wajeruhiwa baada ya basi kugonga kichwa cha treni.

Mtu moja amefariki duni na wengine 38 wamejeruhiwa baada ya basi la Bunda kugonga kichwa cha treni  katika makutano ya reli na barabara wilayani Manyoni.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo imehusisha basi la Bunda lenye usajili wa namba T 782 BKZ lililokuwa likitokea mkoani Dodoma na kuelekea  mkoani Mwanza, mkuu wa wilaya ya Manyoni bi Fatuma Toufiq amesama ajali hiyo imetokea majira ya asubuhi saa mbili tarehe 28  katika makutano ya barabara na reli mjini Manyoni.
Akiongea na ITV  na Radioone muuguzi mkuu wa haspitali ya  wilaya ya Manyoni Bi. Heliechi Malisa amesema wamepokea maiti  moja ambayo imetambulika kwa jina la Perina Bikombo mkazi wa Manyoni na majeruhi thelasini na nane  wamelazwa na wanapatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Manyoni.
IANGALIE VIDEO HAPO CHINI,
SOURCE:-ITV NEW'S

No comments: