Tuesday, 25 February 2014

Rais Yoweri Museveni aidhinisha sheria kali dhidi ya ushoga nchini Uganda

Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameidhinisha sheria mpya ya wapenzi wa jinsia moja.
Akitia saini mbele ya waandishi wa habari na mawaziri waliokuwa wanashangilia, amesema masuala ya wapenzi wa jinsia moja yamechochewa na makundi ya mataifa ya magharibi yalio na kiburi.
Wakati huo huo makundi ya kutetea haki za wapenzi hao yameshutumu vikali hatua hiyo ya Rais Museveni.
 Mswada huo unaotoa adhabu kali kwa watakaopatikana wakishiriki mapenzi ya jinsia moja. Haya yanajiri huku kikundi cha watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja nchini Kenya wakiandamana  jijini Nairobi, wakitaka kutambuliwa na katiba ya Kenya. Sheria hiyo mpya ya uganda inatoa adhabu ya kifungo cha miaka 14 jela kwa wale watakaopatikana kwa mara ya kwanza au kufungwa maisha kwa kushiriki kitendo hicho.

No comments: