Wednesday, 5 February 2014

SHEHENA YA MADAWA YA KULEVYA{HEROIN}YAKAMATWA BANDARI YA DAR ES SALAAM.

ZAIDI ya kilo 200 za madawa ya kulevya aina ya Heroin yamekamatwa na kikosi cha polisi wanamaji katika Bahari ya Hindi yakisafirishwa kutokea nchini Iran pamoja na mabaharia kumi na wawili kutoka nchi ya Iran na Pakistan.
Kamanda wa polisi kikosi cha wanamaji Mboje Kanga ameeleza kuwa tukio hilo lililotokea usiku wa tarehe 4 majira ya saa sita usiku ambapo waliweza kukamata jahazi hilo na mabaharia kumi na mbili wote wakiwa hawaijui lugha ya Kiswahili wala Kiingereza na jahazi lao halikuwa na utambulisho wowote wa sheria za majini.
 Mkuu wa kitengo cha kudhibiti dawa za kulevya, Kamanda Godfrey Nzowa amesema jahazi hilo liliweza kukamatwa baada ya kikosi cha polisi cha wanamaji kuendelea na operesheni zake za doria majini na mara baada ya kulitilia shaka waliweza kulikamata na baada ya kulikagua walikamata shehena hiyo ya madawa ya kulevya aliyoyataja kuwa ni aina ya Heroin ambayo mengi huzalishwa nchini Iran & Pakistan.
SOURCE:-ITV.

No comments: