Thursday, 6 February 2014

WAJUE BAADHI YA WASANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA{BONGO FLEVA} NA WATOTO WAO.

SHETTA a.k.a SHETTA THE DON #KINGMSWATI
Shetta anamtoto mmoja wa kike kwa jina la Qayllah. Alizaliwa mwaka 2012 na tumeanza list hii na shetta kwasababu jamaa aliamua kumpa mtoto wake gari aina ya Opa mwaka 2003 rangi ya Silver siku chache baada ya kuzaliwa.”Nisingependa mwanangu akodishiwe Tax au kudandia lift kwenye gari za watu wakati wa kupelekwa clinic na sehem mbalimbali….hivyo ndio maana nikaamua kujidhiki na kumnunulia binti yangu gari hii na pia kuudhihirishia uma ni kiasi gani nampenda na kumthamini mwanangu kipenzi”  alisema shetta.
MWANA FA a.k.a BINAMU
Mwana Fa ana mtoto wa kike anayeitwa Maleeka ambaye alitimiza miaka miwili mwaka jana.“Nimekuwa very careful, I am worried, siko reckless kama nilivyokuwa. Naogopa nina mtu ananitazama na sitaki kumwangusha. Watu wengine tumekua kidogo juu juu sana, sitaki maisha yangu ambayo mimi nimekua impitie mwanangu hata kidogo,”  alisema FA kwenye birthday ya mtoto wake.
ALI KIBA a.k.a ALI K-4REAL.
Ali kiba naye ana mtoto wa kiume ingawa hapendi sana kumzungumzia kwenye mitandao.
MR,BLUE a.k.a BYSER
Mr.blue na mchumba wake waheeda wamekua pamoja kwa miaka 10 sasa na along the way walipata mtoto anayeitwa kherry.“it feels great to be a father , in fact the greatest moment in my life was the day kherry was put on my arms. Nilikua na hisia zisizoelezeka”. Blue alisema kuhusiana na ujio wa mtoto wake huyo kipenzi.

BARNABA a.k.a BARNABA BOY
Msanii Barnaba naye ana mtoto wa kiume anayeitwa steven na kama ulikua haujui,  jina hilo Barnaba alilompa mwanae ni kwa ajili ya kumuenzi mkali wa bongo movies  marehemu steven kanumba "The Great".
GELLY WA RHYMES
Gelly wa rhymes naye ana mtoto wa kike anayeitwa queen





No comments: