Thursday, 6 February 2014

MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA{BONGO FLAVA}AWACHANGANYA KIMAPENZI JACKLINE WOLPER & KAJALA MASANJA.

MSANII wa muziki wa kizazi kipya anayeunda kundi la Makomandoo Fredy Wayne ambaye alikuwa akitoka kimapenzi na muigizaji Filamu wa kike nchini Jacqueline Wolper, amesema ameachana naye na sasa yupo na nyota mwingine wa filamu, Kajala Masanja. Akizungumzia  hilo hivi karibuni, Fredy alisema msanii huyo {Kajala}amemchanganya mno kimapenzi kiasi kwamba ameamua kumwandikia wimbo unaitwa "Ushaniroga", hii ni katika kuonyesha ni jinsi gani amedata na Mbongo movie huyo.
kajala masanja.

“Siyo siri jamani ndiyo kashaniroga, nampenda na yeye kaonyesha upendo wake kwangu, nipo naye na kuhusu huyo Jack Wolper ni maisha tu, ni rafiki zangu, huwa naonana nao katika maeneo tunapiga kiss, ni vitu vya kawaida lakini sasa niko na Kajala,” alisema Fredy Wayne.
Hata hivyo, wadada hao wawili wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo hawakuweza kupatikana ili kuzungumzia habari hiyo ambayo ni gumzo linalofukuta chini kwa chini ndani ya jiji la Dar es salaam kwa hivi sasa.
awali wiki kadhaa zilizopita mwanadada Jackline Wolper alimtambulisha rasmi mchumba wake mpya wa sasa na kusisitiza wako katika hatua za kutaka kuvishana pete na hatimaye MUNGU akibariki wawe Mke na mume.

jackline wolper

No comments: