Thursday, 27 February 2014

WALICHOZUNGUMZA OSTAZ JUMA NA PNC BAADA YA PICHA NA VIDEO ZA PNC AKIOMBA RADHI KUZUA GUMZO

Jumatano (February 26, 2014), Boss wa Watanashati Ostaz Juma alipost picha kwenye ukurasa wake wa Facebook ikimuonesha PNC akimpigia magoti kumuomba msamaha na kuandika “hahaha jamani mziki ni kazi pnc arudi kuomba msamaha ili aendelee kufanya kazi mtanashati”. Kitendo ambacho kilipondwa na wengi na kuonekana kama ni udhalilishaji.

Kupitia ‘The Jump Off’ ya 100.5 Times Fm, Ostaz Juma alieleza sababu zilizompelekea yeye kupost picha hiyo ambapo alidai kufanya hivyo ili kuwaonesha watanzania kuwa malalamiko ya PNC ya awali hayakuwa ya kweli, na kwamba kama yangekuwa ya kweli basi asingerudi tena na kumpigia magoti.

“Watanzania wanaona kama tunawazurumu wasanii ama tunawanyanyasa. Ndio PNC kunipigia magoti na kuniomba radhi, lakini sasa mimi nikaamua kuwaonesha watanzania kwamba PNC amerudi kweli kuniomba msamaha. Je, kama kweli PNC alikuwa analalamika ‘Ostaz anafanya kazi zake hanijali hanisaidii…’- Ostaz Juma.
“Mimi kitu ambacho kinachoniumiza zaidi ni kile ambacho wasanii ukishawasaidia wakasimama wanaonekana, wanaanza kuwa wanafanya vitu vibaya wanasnitch yaani wanadharau na tabia mbovu wanamdharau boss wao na ndio maana nikawa nimekataa baadhi ya wasanii wote.” Aliongeza.
Hata hivyo pamoja na kumuomba msamaha na kumpigia magoti, Boss huyo wa Watanashati Entertainment ameendelea kumkazia uzi PNC na kumpa masharti mengine ili aweze kukubaliwa.
“Lakini kweli PNC karudi kuja kuomba msamaha na mimi nikampa option, kama akitaka nimsamehe lazima arudi kwenye vyombo vya habari kama alivyoenda mwanzo, akawaombe msamaha watanzania na aniombe mimi msamaha kupitia vyombo vya habari ndio mimi ntamsamehe.” Ananukuliwa Ostaz Juma.

Nae PNC alifunguka ya moyoni pia kupitia The Jump Off ya Time Fm, na kwa mujibu ya maelezo yake utagundua ule msemo wa ‘mtaka cha uvunguni…’ unachukua nafasi. PNC anaona kila kilichofanyika kwake kiko sawa tu ili mradi mambo yake yaende.
“Mimi naweza nikasema ni kawaida tu, kwa sababu kuomba msamaha pia ni kitu cha kawaida sio tatizo. Mimi nimefanya hivyo kwa maana yangu tu najua mwenyewe nimefanya hivyo kwa sababu bado nahitaji kufanya kazi zangu ziende. Kwa hiyo sasa nikisema niwe kiburi nini…japokuwa sijakosa mimi ila mkubwa anapoona kuna makosa akawajumlisha wote inabidi mjishushe saa nyingine, ujichukulie kama mdogo sio na wewe unaanza kuwa una viburi na jeuri. Nimeshakaa kwenye game…muziki nimeuanza muda najua madhara yake ni yapi. Kwa hiyo nimefanya tu kawaida kumwambia bwana mambo haya yaishe na nini tufanye mambo yetu.
“Kwa sababu yeye mwenyewe kitu kilichokuwa kinaongeleka kwake ni lawama zake kwamba mimi nilimletea watu, mwisho wa siku wamekuja kuharibu mambo yake mpaka wanafikia hatua ya kufanya mambo mengine wanamkana na nini. Sasa mimi ukiangalia ukweli mimi ndiye niliyewakaribisha wasanii wote waliokuwa Mtanashati. Lakini sio kwamba mimi ndio niliyekosea kwamba nilikosea…mimi sikugombana na Ostaz ila niliona kimya nikaanza kuona hapa kazi hazieleweki nikaamua kusema kama vipi siko Mtanashati. Ila mwisho wa siku nikaa kuongea nae nikajua tatizo liko wapi. Kwa hiyo ikabidi nimweleze bana kama vipi basi tusameheane mambo hayo yaishe tufanye kazi.
“Ukiangalia kwenye hizi picha, nimeziona hizi picha na kuna watu wanaandika mambo yao ya ajabu ajabu wanadiss, lakini mimi naona sawa tu kwa sababu kupiga goti na kumuomba mtu msamaha sio kwamba umemsujudia yeye ndio Mungu hakuna. Ni kama umeonesha heshima tu kwamba wewe ni brother. Ukiangalia mimi silingani nae umri hata kidogo na huyo mtu ndio mtu ambaye hata kwa ndugu zangu anaongea nao.
“Kwa hiyo fresh tu nimeomba samahani kama brother angu. Potelea mbali maneno yataongeleka yataenda yatapita, mimi kazi zangu ntaendelea kufanya.”
SOURCE:-BAABKUBWA MAGAZINE.

No comments: