Tuesday, 18 March 2014

DIAMOND PLATNUMZ NA HATI HATI YA KUFILISIKA.

Ile historia ya mfalme wa TAKEU nchini Lucas Mkenda a.k.a Mr Nice inaweza kujirudia tena kwa sukari ya Warembo, mkali wa bongo fleva Nasib Abdul “Diamond Platnumz“ habari za uhakika zinaeleza kwamba utajiri wa Diamond umepungua kwa kiasi kikubwa sana tofauti na  inavyosemekana kwenye vyombo vya habari hapa nchini kuwa Msanii huyo ana mali nyingi sana lakini watu wake wa karibu wanasema kuwa hakuna ukweli kwenye habari hizo.

Diamond amewahi kutajwa kuwa ndiyo msanii mwenye utajri wa billion moja au zaidi kwa vigezo vya kuwa na nyumba nyingi alizonunua, miradi kibao aliyofungua na mtaa alioununua katika kitongoji cha kijitonyama jijini Dar-es-salaam.
Ila cha kushangaza ni kwamba kwa Kipindi chote Diamond amekuwa anaishi kwenye nyumba za kupanga na nyumba iliyodaiwa kuwa ya Diamond ni Nyumba iliyoko Mwananyamala lakini kwa mujibu wa watu wanaomfahamu Diamond wanasema kuwa Nyumba hiyo inahitaji marekebisho makubwa sana ili nyumba hiyo iweze kuwa nyumba ya mtu mwenye hadhi ya utajiri wa billion 1, habari kutoka ndani ya Kitongoji cha Mwananyamala yenyewe ni kwamba hakuna mtaa alioununuwa mkali huyo.wala hakuna Mtaa unaojulikana kwa jina la Diamond.
Taarifa zinadai kuwa Diamond huwa anatabia ya kuazima magari ili kuonekana ni la kwake kipindi cha karibuni inasemekana alipewa gari na mfanyabiashara maarufu hapa nchini Mohamed Kiumbe “Chief Kiumbe” huku gari hilo akilichukua kwa nia ya kutaka kulinunua siyo kupewa kama alivyosema yeye kama "kaka yake kampa gari aina ya VX V8 yenye thamani ya million 250".

SOURCE:-BAABKUBWA MAGAZINE.

No comments: