Mwanamuziki wa muziki wa kufoka au Rap nchini
Marekani Kanye West, hajakana wala kukubali mashitaka ya kumshambulia
mpiga picha katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Los Angeles.
Adhabu yake ni kifungo cha nje kwa miaka miwili
na pia KANYE,ameshurutishwa na mahakama kupata ushauri nasaha kuhusu anavyoweza
kudhibiti hasira zake. Kutokana na hukumu hiyo KANYE ametakiwa kuhudumia jamii kwa masaa 250 hii ni kutokana na kosa
hilo alilofanya Julai mwaka jana.Mpiga picha {Paparazzi },Daniel Ramos, alimtuhumu muimbaji huyo kwa kumpiga makonde na kumpokonya kamera yake.
Muimbaji huyo mwenye umri wa miaka 36 anasisitiza kuwa hana hatia.
![]() |
Daniel Ramos |
"nilikuwa nafanya kazi yangu wakati West aliponishambulia, '' alisema mpiga picha huyo, '' ikiwa ni mimi ningekuwa nimemfanyia kitendo hicho ningekuwa kizimbani.''
Ramos pia alidai kuwa alihofia kulipiza kisasi baada ya matamshi ya muimbaji huyo kupitia kwenye televisheini.
West alikamatwa mwaka 2008 kufuatia vurumai lengine na mpiga picha katika uwanja huohuo wa ndege.
Kesi hiyo, ilitupiliwa mbali na mahakama baada ya West kuwalipia vifaa vilivyoharibika na pia kupata ushauri nasaha kuhusu namna ya kudhibiti hasira zake.
SOURCE BBC-SWAHILI.
No comments:
Post a Comment