Tuesday, 4 March 2014

Lupita Nyong'o anyakua tuzo ya Oscar

Kama ilivyokuwa imetarajiwa na wengi muigizaji mashuhuri kutoka nchini Kenya Lupita Nyong'o amenyakuwa tuzo za Oscar kwa muigizaji msaidizi wa kike kwa jukumu lake la kuelezea masahibu ya Patseh katika filamu ya utumwa ya ''12 Years A Slave.''

Baada ya kupokea tuzo hilo Lupita amesema " Haikwepi mawazo yangu kwamba hata dakika moja ya furaha katika maisha yangu ni shukrani na maumivu makubwa kwa mtu mwingine.''
Kisha Lupita akaongeza kusema, " Na iwe ukumbusho kwangu na kila mtoto kwamba kokote unakotoka, ndoto zako ni halisi.''

 Mwigizaji Jared Leto alinyakuwa tuzo la mwigizaji bora msaidizi wa kiume kwa jukumu lake la kuelezea maisha ya mwanamke aliye na jinsia mbili aliyekuwa akiishi na virusi vya HIV katika filamu Dallas Buyers Club.


Alilazimika kupunguza uzani kwa kipindi kifupi ili kuigiza.
Sherehe ya kutolewa kwa tuzo hizo zimefanyika mjini Los Angeles nchini Marekani.
Hii hapa ni Video ikionyesha jinsi LUPITA NYONG'O alivyotangazwa mshindi wa tuzo hizo za OSCAR ikiwemo hotuba fupi toka kwake,

No comments: