Mtangazaji maarufu wa Runinga Bongo, Maimartha Jesse amejikuta akiwekwa
nyuma ya nondo kwa madai ya kumtapeli dada mmoja aliyetambulika kwa jina
moja la Zai, mkazi wa Zanzibar,
Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa, mtangazaji huyo alilipwa pesa ya kianzio cha shughuli ya u-MC visiwani humo mwezi mmoja uliopita lakini akashindwa kwenda bila sababu za msingi.
“Kiufupi Maimartha alifanya usanii, alimzungusha yule dada,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya siku ya tukio kupita na Maimartha kuingia mitini, chanzo hicho kilisema Machi 4, mwaka huu, Zai alimfungia safari Maimartha hadi Dar na kumpeleka Kituo cha Polisi Oysterbay kabla ya wawili hao kumalizana.
Alipotafutwa Maimartha kuzungumzia juu ya sakata hilo, alitiririka: “Imeniuma sana, kiukweli alinipa fedha za kianzio huyo dada (Zai) lakini nilishindwa kwenda Zanzibar kwa sababu nilipata dharura, hata hivyo nimeshangaa amekwenda kupandisha dau kule polisi tofauti na fedha ndogo aliyonipa, sitaki kuongelea sana lakini nashukuru yameisha.”alisisitiza Maimartha.

No comments:
Post a Comment