MWANAMUZIKI mkongwe nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ anayetumikia
kifungo cha maisha jela na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ kwa
Kosa la kuwanajisi watoto tisa, wanayo furaha upya baada ya mwanga wa kuweza
kurudi uraiani kuchomoza tena, wakili wao, Bw,Mabere Nyaucho Marando
amezungumza na Gazeti la Uwazi
“Kuna kesi mahakama kuu kanda mojawapo nchini,Kesi inayotetewa na wakili maarufu
(jina tunalo). Hii kesi inafanana sana na ya akina Babu Seya. Uzuri
wake ina dalili zote za washtakiwa kuibuka na ushindi wa kishindo.
MAHOJIANO
Mazungumzo kati ya Marando na Gazeti la Uwazi yalikuwa hivi:
Uwazi: Lakini mheshimiwa kesi ya Babu Seya si ilifika katika rufaa mara tatu na wakashindwa na ulisema hakuna namna tena, sasa itakuwaje kurejeshwa tena huko?
Uwazi: Lakini mheshimiwa kesi ya Babu Seya si ilifika katika rufaa mara tatu na wakashindwa na ulisema hakuna namna tena, sasa itakuwaje kurejeshwa tena huko?
Marando: Ni kweli, lakini ni jambo linalowezekana.
Nimesema kama hiyo kesi ninayoitaja watashinda na wanaweza kushinda, basi mimi nitaenda kwa Nguza na kumwambia wazo langu, akikubali nitaiandikia barua mahakama ya rufaa kuomba kupitiwa tena kwa yale mashitaka, nitajenga hoja.
Uwazi: Hiyo kesi unayoingoja hukumu yake inahusu nini?

Marando: Inahusu kubaka na kulawiti, ni kama hii ya Babu Seya na wanawe.
Hakuna tofauti. Sasa washitakiwa wale wakishinda ndipo hoja inapokuja,
kwa nini vipengele vilevile viwatie hatiani akina Babu Seya wengine
viwaweke huru, ndivyo inavyokuwa katika kesi.
Uwazi: Ukiwaandikia
mahakama ya rufaa wakakubali, majaji walewale watasikiliza ombi lako?
Marando: Hilo ni la mahakama lakini idadi inaweza kuongezwa na kufikia
majaji sita au saba.Uwazi: Una hakika utashinda na kukubaliwa?
Marando:
Kama nilivyokueleza, ikipita ile kesi halafu mahakama ya rufaa
wakakubali kupitia tena jalada, nina uhakika wa kushinda.
ANALIPWA NA NANI?
Wakili huyo maarufu alisema yeye aliwatetea wanamuziki hao bure kwenye
kesi yao ikiwa katika ngazi ya mahakama ya rufaa baada ya kusoma jalada
lenye kurasa 1,362 ambapo aligundua kuwa kuna nyaraka kadhaa ambazo
hazikuambatanishwa katika Mahakama ya Kisutu ambazo zingeweza kuwaokoa
na kifungo wateja wake.
“Unajua kesi inapokuwa mahakama ya rufaa, majaji wanachofanya ni kupitia jalada si kusikiliza, hivyo haiwezekani kuambatanisha vielelezo vipya,” alisema Marando ambaye anajipambanua kuwa awali alishinda nusu kwa kuwatoa nje watoto wa Babu Seya, Mbangu na Francis Nguza ambao nao walihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa moja na wafungwa hao.

HUKO NYUMA
Juni 25, 2004 Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam,
Addy Lyamuya aliwatia hatiani kwa ubakaji na ulawiti Babu Seya na wanawe
Papii Kocha, Mbangu na Francis. Januari 27, 2005, Jaji wa Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao
iliyokuwa ikipinga hukumu hiyo.
Wakili Marando akapeleka suala hilo Mahakama ya Rufaa Tanzania ambako Mbangu na Francis waliachiwa huru na yeye kutangaza kwamba ameshinda nusu. Babu Seya na wanawe walidaiwa kutenda makosa 10 ya kubaka na kulawiti watoto hao kati ya Aprili na Oktoba 2003 katika maeneo ya Sinza ya Kwa remmy, jijini Dar es Salaam.

SOURCE-GPL
No comments:
Post a Comment