Friday, 14 March 2014

OMMY DIMPOZ"VIDEO SHOOTING PHOTOS"IN {UK}

Picha kadhaa za scene katika Video mpya yake Ommy Dimpoz zikimuonyesha Ommy Dimpoz akiwa chini ya ulinzi nchini Uingereza, Hii ni Video iliyosimamiwa na  Director maarufu ambaye amefanya video za wasanii wakubwa Africa na Video hizo zikafanya vizuri,Director "Mr Moe-"Musa" Video alizofanya Director huyo wa Video hii mpya ya Ommy Dimpoz,ni Video za wasanii kama Fuse ODG, Davido na Wizkid. Hii ni hatua nyingine kubwa kwa Ommy Dimpoz katika kuupeleka mbali zaidi muziki wake na kuiletea sifa na mafanikio TANZANIA hasa ukizingatia Ommy Dimpoz ni Msanii mwenye nyimbo tano tu alizoziachia kwenye radio mpaka sasa nchini Tanzania.ambazo ni "nai nai"{Feat ALI KIBA},"baadae","me n you{Feat VANNESA MDEE},"tupogo"{Feat J'MARTINS}& "miss-koi-koi{ambayo ndiyo Ngoma yake mpya kwa sasa}
 Kwa taharifa Video hii inatarajiwa kumalizika na kuachiwa mwishoni mwa mwezi huu ambapo pia inatarajiwa kuwepo kwenye chanel nyingi na kubwa kutokana na Director na ufanywaji wa Video hii ambapo vifaa vilivyotumika ni modern na vyenye gharama ya juu sana ikiwemo Camera RED pamoja na professional FILM crew nzima waliotumika kushoot video hii.
Video hii imemgharimu OMMY Dimpoz si chini ya $20,000 za kimarekani ambazo ni kiasi pekee alichomlipa Director huyo huku ukitoa gharama zake nyingine zilizotumika kwenye kusafiri toka sehemu moja hadi njyingine kwa ajili ya utengenezwaji Video hiyo,hii ni pamoja na kuwepo nchini Uingereza kwa kipindi kizima cha utengenezaji wa video hiyo.

Na Hizi basi ndizo baadhi ya picha zilizopigwa wakati wa uchukuaji kichupa hicho nchini Uingereza,


No comments: