Katika
hali isiyokuwa ya kawaida,Mashabiki wa timu ya Simba wameanza tena
kung'oa viti vya kukalia uwanjani hapa na kuwatupia Mashabiki wenzao wa
Timu ya Yanga waliofurika kwa wingi uwanjani hapa,kwa kile kinachodaiwa
kuwa hawataki kukaa nao sehemu moja.lakini kwa hali ilivyo hivi sasa
Uwanjani hapa,ni dhahiri kabisa kuwa Mashabiki hao wa Yanga wanaweza
kuujaza Uwanja huu hasa kwa jinsi wanavyozidi kuingia Uwanjani
hapa.Uongozi wa Vilabu hivi viwili vikubwa hapa nchini unatakiwa kukaa
chini na Mashabiki wao na kuwakanya kuhusiana na uharibifu wa
Miundombinu wanaoufanya Mashabiki wao katika Uwanja huu wa Taifa,kwani
kuendelea kwa vitendo hivi kunazorotesha sana soka letu.Picha zote na
Othman Michuzi,Uwanja wa Taifa jijini Dar.
No comments:
Post a Comment