Ndoto za mabingwa wa soka Tanzania bara,Da Young Africans{Tanzania} kutinga hatua
ya 16 bora katika michuano ya Soka klabu Bingwa barani Afrika,imefikia
ukingoni baada ya kutolewa kwa mikwaju ya penalti 4-3 na Al Ahly ya Misri siku ya jana jumapili usiku mjini Alexandria{Misri}.
Katika Mechi hiyo hadi dakika tisini zinamalizika wenyeji Al ahly walikuwa wameshinda bao 1-0, hali iliyolazimu kutumika sheria ya mikwaju ya penalti kufuatia ushindi wa Yanga wa bao 1-0 katika mechi ya awali jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.
Haikuwa siku ya bahati kwa Yanga baada ya awali mlinda mlango wake Deogratias Munisi almaaruf kwa jina la"Dida" kupangua mikwaju miwili kati ya mitano ya awali toka kwa AL AHLY, ila wapigaji wa penalti Kwa upande wa Yanga walishindwa kutumia fursa vizuri kujaza mipira nyavuni, ambapo penalti ya mwisho iliyotaraji kuwavusha Yanga ilitolewa nje na mpigaji Said Bahanuzi, na hivyo kukamilisha penalti tano tano,kila timu ikiwa imekosa penalt mbili mbili.
Katika penalt za nyongeza Al Ahly walipata penalti ya sita huku Mbuyu Twite wa Yanga akikosa penalti yake muhimu iliyohitimisha safari ya Yanga kwenye michuano hiyo mwaka huu 2014.
Baada ya kuweka historia kwa upande wake kwa kuifunga Al Ahly bao 1-0 katika mechi ya awali jijini Dar es Salaam, Yanga ilikuwa na matumaini makubwa ya kuandika historia nyingine kwa kuilaza Al Ahly iliyokuwa ikicheza nyumbani.
hii ni video inayoonyesha jinsi YANGA ilivyokwama kwenye matuta ya penalti,

No comments:
Post a Comment