MASTAA
mbalimbali nchini wakiwemo wanamuziki wanatarajiwa kushiriki kwenye
tukio maalum la kumbukumbu ya mwaka mmoja tokea kifo cha marehemu
Albert Mangwea ‘Ngwair’ , litakalofanyika ndani ya ukumbi wa Nyumbani
Park (Samaki samaki Spot) , Kihonda Morogoro mjini leo Juni 28.
Akizungumza na
mtandao huu , Mratibu Mtendaji wa tamasha hilo, Kareeem Omary ‘KO’
alisema maandalizi ya tukio hilo litakalokuwa la kila mwaka, lililopewa
jina la ‘Love Concert - Kumbukumbu ya kifo cha Albert Mangwea’
![]() |
| Mratibu Mtendaji wa tamasha hilo la ‘Love Concert –Kumbukumbu ya Mangwea’, Kareeem Omary ‘KO’. |
.
Kareem,
aliwaomba wadau kujitokeza kwa wingi kuunga mkono kwenye tukio hilo
kwani litakuwa la kipekee na la aina yake ambalo pia litatoa fursa kwa
wakazi hao pia mikoa jirani na watu kutoka nje ya Tannzania ambao
watauzuria.
“Nawaomba
wadau kujitokeza kuonesha upendo wa pamoja. Kumbukumbu kwa mpendwa
wetu kama ilivyo utamaduni wetu.” alisema Kareem.
Na kuongeza kuwa, siku hiyo Watu mbalimbali watapata kupiga picha na mastaa pamoja na mama mzazi wa Mangwea kama kumbukumbu.
Kareem
aliwataja wasanii watakaotoa burundani, ni pamoja na kutoka kwa kundi
la Wanachemba ambalo pia aliwahi kuwa nalo marehemu Ngwair, JSqueezer, P
Funky Majani na Mswaki. Kwa upande wa wasanii kutoka Morogoro ni pamoja
na Afande Sele, Team Racers, Mc Koba Chris wa Marya, Belle 9, Samir,
Zombie, President Mirrow, Jordan wa Dejavu na wengine wengi.
Katika siku
hiyo ya Juni 28, ambayo ndiyo siku aliyopatwa na umati marehemu, Kareem
alisema kabla ya matukio ya shoo ukumbini, itatanguliwa na ibada mbili
maalum ikiwemo ya Kanisani na ile ya nyumbani.
Aidha,
Kareem
alisema katika tukio hilo, ambalo linatarajia kuanza majira ya jioni ya
saa 10 hadi saa 12 jioni, wametoa fursa kwa watoto kutoa burudani
ikiwemo ya kuimba na nyinginezo na baadae usiku wa kuanzia saa 2 hadi
majogoo wasanii hao mbalimbali watatawala jukwaa na burudani ya nguvu ya
kumbukumbu.
Marehemu
‘Ngwair’ alifariki dunia akiwa nchini Afrika kusini, alijizolea
umaarufu kwa nyimbo kama Mikasi na Nisikilize Mi na nyingine nyingi
alizowahi shirikishwa na wasanii mbalimbali nchini wakiwemo Professa
Jay, Nuru, TID, Chidi Benz na wengine wengi.
![]() |
| Taswira ya Nyumbani kwa Mama Mangwea kwa sasa. |





No comments:
Post a Comment