Friday, 9 May 2014

LULU ASHAURI WAIGIZAJI MOVIE BONGO WARUHUSIWE KUIGIZA NUSU UCHI ILI KUENDANA NA SOKO KIMATAIFA.

Muigizaji maarufu wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameziomba mamlaka husika zinazosimamia maadili ya filamu nchini ziwaruhusu wasanii Waigizaji Filamu nchini waigize nusu utupu ili kuendana na soko la kimataifa.
Akitetea hoja yake , staa huyo aliyeitendea haki filamu yake ya Foolish Age alitolea mfano Tamthiliya ya Shuga iliyomtoa na kumpa umaarufu zaidi muigizaji na mwanamitindo maarufuu kwa sasa duniani toka Africa Lupita Nyong’o ambayo aliicheza akiwa nusu utupu.
“Wanasema hatufuati maadili wakati kuna muvi ambazo zipo "theatre" na watu wanaangalia hazina maadili, wao wanataka tufanye vitu kwa kudanganya wakati sasa hivi tuko dunia ambayo tuna takiwa tuweke vitu wazi, wasibane sana,” alisisitiza Lulu.


No comments: