Friday, 9 May 2014

JOKATE ATOA VIGEZO KWA MWANAUME ATAKAYE KUMUOA.

Jokate.
Mwanamitindo na mmoja kati ya watangazaji mahiri wa Tv-Bongo, Jokate Mwegelo ameibuka na kuanika sifa za mwanaume ambaye anafaa kuwa mume wake mtarajiwa.
Jokate alisema anapenda kuolewa na mwanaume ambaye atajua kutafuta fedha kwa nguvu zake zote, na awe anajua kubembeleza pia awe na nidhamu kwa wazazi wake.
“Sifa ya mume ninayemtaka, anapaswa kuwa mtafutaji wa fedha, sipendi mwanaume asiyependa kutafuta, awe anajituma kwa kazi zake na kwa mpenzi au familia yake na pia ajue kunibembeleza,’’ alifunguka Jokate.

No comments: