Monday, 19 May 2014

PASTA MYAMBA KUFUNGA NDOA AUGUST 2

Pasta Emmanuel Myamba akiwa na Muigizaji mwenzie Monalisa.
Msanii wa filamu nchini{TZ}, Emmanuel Myamba aka Pastor Myamba anatarajia kufunga ndoa na mwanadada Trakseda Kasela,Ndoa itayofungwa August 2 huko visiwani Zanzibar.
Akizungumzia hilo Pastor Myamba amesema kuwa huu ndio wakati wake ambao ameamua kuutumia kufunga ndoa na kukaa na mke wake pamoja.
“Mwezi wa nane tarehe mbili Mungu akinijalia nitakuwa naoa, mke wangu ni wa hapa hapa Dar es Salaam lakini sio msanii, sipendi kuoa wasanii bwana, wasanii mambo mengi,” amesema Myamba. “Mpaka sasa hivi ninatoa tu taarifa nadhani harusi yangu haitafanyikia kanisani na itafanyikia kwenye garden huko Zanzibar. Mpaka sasa hivi bado nipo kwenye maandalizi ya mwisho, kwahiyo msishangae siku ya mwisho nabadili baada ya kwenda kufungia Zanzibar nikafanyia hapa hapa. Lakini kila kitu kipo sawa kwamba natarajia kuoa sasa na kuishi pamoja na mke wangu, ninayetarajia kumuoa anaitwa Trakseda Kasela.”alisisitiza Pasta Myamba.

No comments: