![]() |
Baba Levo |
Msanii wa muziki na mchekeshaji, Baba Levo ambaye sasa ni Diwani wa Mwanga Kaskazini mkoani Kigoma, amebadili uamuzi aliopanga kuuchukua baada ya kushinda nafasi hiyo ya kuwatumikia wananchi, ambao ni kuacha kufanya muziki.
Uamuzi wa kuendelea na kazi ya muziki huku akiwa Diwani umetokana na ushauri aliopata kutoka kwa Mbunge wa Kigoma Mjini mhe. Zitto Kabwe.
Baba Levo ameiambia Bongo5 kuwa Zitto amemshauri asiache kufanya kazi yake ya muziki kwasababu udiwani sio ajira ya kutegemea kuendeshea maisha bali ni uwakilishi wa wananchi. “Nilijaribu kumshaurisha brother Zitto kwasababu yeye ni mzoefu kwenye uongozi, nikamwambia Bro nimeshashinda, sasa kuna vitu kama zile comedy kwa Millard Ayo, pia kuna vitu kama muziki kuna shows na vitu kama hivyo” alisema Baba Levo. Hiki ndicho Zitto alimjibu, “…akasema hapana usiache kwasababu ile ni talent yako na ile itakuingizia pesa nyingi, kwasababu udiwani hauna pesa na udiwani sio kazi ni uwakilishi unawakilisha wananchi. Lakini unao uwezo wa kwenda kufanya kazi yako na ukarudi kwaajili ya kuendelea kuwakilisha wananchi, ukitoka mara moja hata siku 4 ukaja kuendelea na kazi ya wananchi. Kwahiyo ndio kama hivyo niliondoka nilienda Katavi kufanya show zangu, nimerudi naendelea na kazi huku saizi niko njiani naelekea kwaajili ya kwenda kufanya usafi wa soko.” alieleza Baba Levo.
Baba Levo ameongeza kuwa ana mpango wa kufungua studio Kigoma atakayoitumia kurekodi nyimbo zake, lakini pia atakuwa akisafiri kwenda kurekodi kwenye studio zingine na kurudi Kigoma kuendelea na shughuli zake za Udiwani.
No comments:
Post a Comment