![]() |
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis |
Kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya mateso imelaumu
vikali Uongozi wa kanisa Catholiki kwa kutoshughulikia ipasavyo suala la
unyanyasaji wa ngono ndani ya kanisa hilo.
Katika ripoti iliyochapishwa hivi karibuni na
Umoja huo mjini Geneva , Kamati hiyo imeushutumu utawala wa Vatican kwa
kuwahamisha watawa kutoka parokia moja hadi nyingine kuwaepusha
kushtakiwa, na kupuuza haki za waathiriwa za kupokea fidia .Utawala wa Vatican uliidhinisha mkataba dhidi ya unyanyasaji , ukatili na matendo yaliyo kinyume na utu.
![]() |
Vatican inapuuza haki za watoto |
Kamati hiyo ya Umoja wa Mataifa ina hofu kuwa wakati utawala wa Vatican umeelezea kutokubali kamwe kuwepo kwa unyanyasaji ndani ya kanisa, maneno hayo hayaendani na vitendo .
Kamati hiyo imekasirishwa zaidi na kwamba Utawala wa Vatcan unasisitiza kuwa unahusika zaidi na wahudumu wanaofanyia kazi ndani ya Vatcan kwenyewe , kuliko makasisi wake wanaofanyia kazi kwingineko duniani.
Mwezi Januari mwaka huu utawala wa Vatican ulichunguzwa upya na kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watoto, baada ya kupokea ukosoaji kama huo kwamba ulishindwa kuwalinda watoto waliokuwa chini ya uangalizi wake.
No comments:
Post a Comment