Msanii Amini Mwinyimkuu a.k.a "AMINI" toka nyumba ya kukuzia vipaji{THT} juzi alifunga Ndoa kimya kimya bila baadhi ya mastaa wenzake kuhusika na harusi hiyo ambayo wengi wamesema ilikuwa kama ya ghafla.
Miaka kadhaa nyuma Msanii mwingine D.Knob aliwahi kufunga ndoa ya namna hii ambayo kwa maelezo yake alisema kuwa harusi yake hawakuzidi watu 15 kuanzia Kanisani mpaka sehemu waliyoamua kukaa na kupata vinywaji kadhaa.
hivyo Amini amefuata nyanyo za D.Knob na wasanii kadhaa ambao waliwahi kufuga ndoa za kimya kimya kama hii, kwa Amini ndoa yake ilifungwa Msikiti wa Ibazi uliopo Manzese baada ya swala ya saa 2 usiku,idadi ya watu walioshuhudia ndoa hiyo hawakuzidi watu 20 na hiyo ni jumla ya wazazi pamoja na wasindikizaji pia.
Farida Bashir au Namcy Vana ndiye bi harusi na msichana aliyefunga Ndoa hiyo na msanii Amini,ambaye sauti yake imesikika kwenye wimbo unaosumbua sana jijini hasa kwenye shughuli zilizojizolea umaarufu zaidi jijini Dar es salaam Maarufu kama Vigodoro wa Kantangaze uliotoka miezi kadhaa iliyopita,kwa takriban Miaka kadhaa nyuma msanii Amini amewahi kuripotiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii mwezake Linah.
Waweza kubonyeza play hapo chini kumsikiliza Amini mwenyewe kuanzia ndoa wakati inafungwa mpaka ilipokamilika.

No comments:
Post a Comment