June 05 2014
mchana kupitia mitandao mbalimbali Tanzania zilisambaa taarifa
zikimuhusu mmiliki wa mojawapo ya nyumba maeneo ya Sakina jijini Arusha
kwamba nyoka aliyekua akimfuga kwa siku nyingi na kuhusishwa na imani za
kishirikina, ameuwawa na Wananchi.
‘Kusema kwamba
nilikua nafuga kwamba huyu nyoka ni mtoto wangu wa kwanza….. sasa kama
ni mtoto wangu wa kwanza si inamaana na mtoto wangu angekufa na yeye?
mimi nasema namwachia Mungu tu…….. sijawahi kusikia Nyoka kuishi maeneo
hayo toka nimeanza kuishi kwa karibu miaka 8, hata na mimi inanitatiza
manake nimetumiwa picha Nyoka amefungwa kitambaa chenye maandishi
mekundu kama ya kiarabuarabu hivi….
Wananchi
walimuua nyoka huyo na kisha kumkata kata vipandevipande ambapo baada ya
hizi taarifa kusambaa mmiliki wa nyumba hii aliomba kuongea na mtandao
wa millardayo.com ili kutoa maelezo yake ambayo anadai ndio ukweli wenyewe.
Mr. Joseph
Paschal Magesa anasema "Mimi kama mimi kwanza ni Mkristo safi na mzee wa
kanisa na niliondoka nyumbani jana na mke wangu kutoka Arusha kuelekea
Dar es salaam, sijui lolote kuhusiana na hicho kitu ila nilipofika
maeneo ya Mwanga na Same nikapigiwa simu kwamba kuna nyoka huku ndani ya
eneo la garden nyumbani, kuna vijana niliwaacha wawili pale nyumbani
nikawaambia waambieni watu wawasaidie kumuua huyo nyoka’
‘Wakamuita
jirani yangu hapo ndipo nae akanipigia simu nikamwambia bwana wewe si
una bunduki nisaidie kumuua huyo nyoka ila alivyokata simu nilijua
ametekeleza kumbe aliondoka, baadae napiga tena simu nauliza vipi
naambiwa bado yupo na watu wamejaa nikawauliza kwani hao watu hawawezi
kumuua mpaka bunduki wakasema wanaweza ndio baadae wakanambia wamemvuta
mkia wamemuweka nje ya geti’
‘Nikawauliza
anavutika asije akawa analeta shida wakasema anavutika, nikawaambia
mpelekeni kanisani kwa sababu nyumbani kwangu ni jirani na kanisa ndio
wakamvuta hadi kanisani wakammwagia maji ya baraka kisha wakamkatakata
ndo ikawa mwisho wake hapo’.
‘Taarifa
kwamba Nyoka huyu amevunja kioo cha dirisha akiwa anatokea ndani ya
nyumba, sio kweli…. haipo kabisa hiyo kitu eti kwamba ametokea ndani,
hayo ni mambo ya watu tu… hicho kioo nilikifunja mimi wakati napanga
mizigo ya ofisi yangu… sifahamu chochote kuhusu huyu Nyoka, Watanzania
waniamini haya ninayosema ndio yanayotoka moyoni mwangu’
Bonyeza play hapo chini kusikiliza alichokisema zaidi Mr. Joseph Magesa.
No comments:
Post a Comment