Tuesday, 10 November 2015

MAALIM SEIF{CUF} NA Dr,ALI SHEIN{CCM}WAKUTANA KWA TAKRIBAN SAA SITA KUZUNGUMZIA MUSTAKHBALI WA ZANZIBAR.


Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amekutana na kuzungumza kwa saa sita na nusu na mgombea mwezake wa urais kupitia CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kujadili mgogoro wa uchaguzi, baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec), Jecha Salim Jecha, kufuta matokeo.
Uchaguzi huo ulifanyika Oktoba 25, mwaka huu na Jecha alitangaza kuufuta Oktoba 28, kwa madai kuwa kulikuwapo na kasoro kadhaa.
Taarifa zilizopatikana , zimeeleza kwamba kikao hicho kati ya Rais Shein na Maalim Seif, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, pia kilihudhuriwa na viongozi kadhaa wastaafu.
Viongozi hao ni Rais mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi na Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.
Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu ya Zanzibar na kumalizika saa kumi jioni na ajenda kubwa ilihusu mgogoro wa uchaguzi visiwani humo.

No comments: