Thursday, 12 June 2014

JENGUA NA BI,MWENDA FULL MALOVEE MSIBANI.

Muigizaji mkongwe katika tasnia ya filamu Bongo, Mohammed Fungafunga 'Jengua' akiwa msibani kwa aliyekuwa gwiji la vichekesho marehemu Mzee Small
NG’OMBE hazeeki maini! Katika hali ya kushangaza, waigizaji wakongwe, Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’ na Jengua walioneshana malovee msibani kwa kuitana mume na mke. 
.Ishu hiyo ilitokea juzi, Jumatatu kwenye msiba wa nguli wa vichekesho nchini, Said Ngamba ‘Mzee Small’ ambapo paparazi wetu aliwashuhudia wawili hao wakiitana bebi huku wakifuatana kila sehemu.
Muigizaji mkongwe, Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’.
 
alipoulizwa Jengua kuhusiana na ukaribu huo msibani, alisema haoni tatizo kuwa mpenzi wa Bi. Mwenda lakini mama huyo alikataa na kusema labda katika filamu tu

No comments: