Sunday, 1 June 2014

Msiba: Mh,Mbunge Zitto Kabwe afiwa na mama yake mzazi

Marehemu Bi,Shida Salum{Mama Mzazi wa Mh,Zito Kabwe}
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Mh,Zitto Kabwe, mchana huu amefiwa na mama yake mzazi aliyeugua kwa muda mrefu.

Bi Shida Salum, amefariki katika hospitali ya AMI jijini Dar Es Salaam ambako amekuwa akitibiwa kwa zaidi ya wiki mbili.
Awali Bi Shida alikuwa amepelekwa India kwa ajili ya matibabu kabla ya kurejeshwa nchini.
Zitto ni mbunge kijana kutoka CHADEMA, ambaye amepata umaarufu mkubwa kutokana na uhodari wake wa kujenga hoja.
Mama yake wakati wa uhai alikuwa mshiriki katika maswala ya kisiasa, ambapo alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.
Mh,Rais Jakaya.M.Kikwete alipokwenda kumjulia hali hospitalini AMI marehemu Bi,Shida Salum{Mama mzazi wa Mh Zito Kabwe}

Ngessablogspot tunatoa pole kwa Mh,Zitto Kabwe, familia na wote walioguswa na msiba huu.
Tutawaletea habari zaidi zitakavyopatikana.

No comments: