Sunday, 1 June 2014

IRENE UWOYA AKIRI KUTOKA KIMAPENZI NA DANSA WA THT

May 28 kupitia You heard ya XXL Clouds FM ilikuwa ni stori kuhusu uhusiano wa Kimapenzi kati ya Msami {Dansa}wa THT na mwigizaji toka Bongo Movie Irene Uwoya, katika siku ya jana alisikika Msami akikanusha uhusiano huo, lakini mpenzi wake Rehema aliweka wazi kuwa ni kweli Msami ana uhusiano wa kimapenzi na Irene Uwoya.


Siku ya May 29 2014 alitafutwa Irene Uwoya na kuulizwa na Soudy Brown kama ni kweli ana uhusiano wa kimapenzi na Msami na swali la kwanza lilitaka kujua uhusiano wao umekuepo toka lini?
Mahojiano yalikuwa kama hivi:-



Irene Uwoya: Siku nyingi’

Soudy Brown: Msami kama namuona, unampa huduma zote?

Irene Uwoya: ‘Sanaaa kila kitu’

Soudy Brown: Uhusiano wenu utadumu au ndio kama wa Ndikumana?

Irene Uwoya: ‘Yakudumu kwa sababu nampenda’.

Soudy brown alimpa Irene taarifa kuwa mpenzi wa zamani wa Msami amekasirika kwa sababu Irene kaingilia mapenzi yao jibu kutoka kwa Irene likawa ‘hiyo haijalishi kwa sababu nampenda

No comments: