![]() |
| Wapiganaji wa madhehebu ya Sunni |
Wapiganaji wa madhehebu ya Sunni wamekishambulia
kiwanda kikubwa mno cha kusafisha mafuta katika mji wa Baiji, Kaskazini
mwa Iraq kwa kutumia mizinga na makombora.
Duru zasema kuwa walinzi watano wa Iraq wameuawa katika shambulio hilo.Kuna habari kuwa Majeshi ya Iraq pia yalituma ndege yake ya Helikopta, ambayo kwa bahati mbaya imelipua tenki moja kubwa ya kuhifadhia mafuta kwa kombora na Kusababisha moto mkubwa.
![]() |
| Kituo cha kusafishia mafuta kilicho shambuliwa |
Makabiliano pia yameshuhudiwa katika mji wa Ramadi Mashariki mwa nchi hiyo.
![]() |
| Wapiganaji |
Serikali inakabiliana na wapiganaji wa ISIS na washirika wake wa Sunni Muslim katika miji ya Diyala na Salahuddin baada ya wapiganaji kuvamia mji wa pili Mosula kwa mara ya kwanza wiki jana.
Waziri mkuu Nouri al-Maliki, alionekana kupitia televisheni na viongozi wa Sunni na wakurdi Jumanne ili kutoa wito wa amani na umoja huku wapiganaji wakijiandaa kwa vita zaidi.
Wanataka watu wanaomiliki silaha na ambao sio wanajeshi wa serikali kusalimisha silaha hizo.
![]() |
| Wapiganaji wa Sunni walliojitolea kupigana |
Mamia ya watu wameuawa tangu mapigazo kuzuka nchini humo wiki jana , wengi wakiaminika kuwa wanajeshi waliotekwa nyara na kupigwa risasi na wapiganaji wa ISIS.
Wakati makabiliano yalipokuwa yanaendelea mjini Baquba, wafungwa 44 waliuawa ndani ya kituo cha polisi katika hali ya kutatanisha




No comments:
Post a Comment