![]() |
| Bw,Andy Coulson |
Aliyekuwa mhariri wa gazeti moja nchini
Uingereza Andy Coulson ambaye baadaye alihudumu kama mshauri wa waziri
mkuu wa Uingereza David Cameron amehukumiwa kifungo cha miezi 18
gerezani kwa makosa ya udukuzi wa mawasilioni ya simu.
Wiki iliyopita Coulson alipatikana na hatia ya kudukuwa mawasiliano ya simu alipokuwa mhariri wa gazeti la News of the World.Gazeti hilo baadaye lilifungwa kutokana na shinikizo kutoka kwa umma nchini Uingereza kufuatia kashfa hiyo ambapo simu za famiia za kifalme, za wanasiasa, na za watu mashuhuri na watu wa kawaida zilidukuliwa.
Kufuatia hukumu hiyo, waziri mkuu wa Uingereza aliomba msamaha kwa kumteua Coulson kuwa mshauri wake.
Waandishi wengine wa zamani pamoja na mchunguzi wa kibinafsi Glenn Mulcaier walikiri kufanya udukuzi wa mawasiliano ya simu na walipewa hukumu ndogo.

No comments:
Post a Comment