Tuesday, 8 July 2014

HII NDIYO SURPRISE DIAMOND ALIYOMFANYIA MAMA YAKE KATIKA SIKU YAKE YA KUZALIWA.

Diamond Platnumz...
Diamond Platinumz amemzadia mama yake mzazi gari aina ya Toyota Harrier Lexus katika siku yake ya kuzaliwa akiwa anatimiza miaka 55, jana (July 7).
Kwa mujibu wa Meneja wake Babu Tale, gari hilo limegharimu kiasi  cha shilingi milioni 35, lakini zilizoongezeka ni shilingi milioni 3.1 kwa ajili ya kulipamba kabla ya kumkabidhi rasmi.
Mama Diamond alikabithiwa rasmi gari hilo mbele ya watu mbalimbali waliofika nyumbani kwao Sinza kwa ajili ya kumpongeza kwa siku ya kuzaliwa na pia kuzindua video mbili za Diamond, MdogoMdogo na Bum Bum, matukio yaliyoambatana na futari ya pamoja ya jioni.
Mama Diamond muda mfupi baada ya kukabidhiwa Gari alilozawadiwa na mwanae.
Ingawa hayupo Tanzania lakini hakungoja mpaka arudi ndipo akabidhi zawadi hii badala yake alichokifanya ni mara baada ya kukamilisha kila kitu kinachoihusu gari hii Diamond Platnumz aliwapatia mameneja wake kwa ajili ya kuiwasilisha kwa mama yake.
Gari alilozawadiwa Mama Diamond na mwanae likionekana pamoja na namba yake ya usajili.
Zawadi hii ameitoa Diamond kwa mama yake kama zawadi kwa ajili ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa mama yake ambaye amesema ametimiza miaka 55, mama yake amesema hakutegemea zawadi hii na anamuombea mwanae kwa Mungu afanikiwe zaidi.
Baada ya kufuturu Meneja wa Diamond Babu Tale alitangaza utaratibu wa kuzindua kwanza video mbili za Diamond kwa watu waliokuwepo hapo,
Huku Babu Tale akifunguka kuwa video hizo ziliwagharimu jumla ya dola 78 ambazo ni sawa na shilingi milioni 130 za Tanzania hadi kukamilika kwake. Amesema video ya Bum Bum iligharimu kiasi cha dola za kimarekani 38,000 na MdogoMdogo iligharimu dola 40,000 za kimarekani.
 kisha utaratibu mwingine ukaendelea ikiwemo kumuimbia mama yake Diamond kisha kukabidhiwa gari yake.
Hizi ni picha kuanzia wakati wa kufuturu hadi mama yake Diamond anakabidhiwa gari hiyo mbele ya mastar kadhaa akiwemo Wema Sepetu,Shettah,Madee,Profesa Jay,Aunt Ezekiel na wengine kibao.
Gari alilozawadiwa Mama Diamond na mwanae...
Waalikwa wakipata Futari....


Babu Tale....

Profesor Jay....

Baadhi ya Waalikwa...


Wema Sepetu...


Wema Sepetu na Mashosti zake.


Futari...
 
 
NB:-HII HAPA POST ALIYOITUMA DIAMOND PLATNUMZ KWENYE PAGE YAKE YA FACEBOOK,POST ILIYOAMBATANA NA VIDEO IKIONYESHA KWA SEHEMU TUKIO LILIVYOKUWA,

No comments: