Monday, 21 July 2014

JANUARY MAKAMBA AMJIBU ASKOFU MOKIWA

January Makamba 
NAIBU Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
January Makamba, amesema hawezi kubishana na Askofu
Mkuu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania,
Valentino Mokiwa, kwa sababu ni kama baba yake.
January aliyasema hayo jana wakati akizungumza na
kituo kimoja cha redio jijini Dar es Salaam. January
ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli mkoani Tanga (CCM),
alisema iwapo Askofu Mokiwa kwa mtazamo wake anaona
staili ya unyoaji nywele ni sifa ya urais basi anawaachia
waumini wake na Watanzania kupima wenyewe kauli
hiyo .

askofu mokiwa.
 Mbali na Mokiwa pia January alitumia nafasi hiyo
kujibu kauli ya Rais Kikwete ambaye alimpa ushauri wa
kusikiliza ushauri wa wazee kabla ya kufanya uamuzi
wake. “Wako wazee wengi ndani ya CCM wa kuwaona na
wengine nimekwishawaona na Rais Kikwete kwa nafasi
yake ni refarii wa mchezo,” alisema January. Alisema
kutangaza kwake kugombea si kwamba anataka cheo cha
urais kwani kwake urais ni utumishi.
January alitoa kauli hiyo siku moja baada ya Askofu
Mokiwa kuzungumzia sifa za mgombea urais akisema
nchi haiko tayari kuongozwa na wanyoa ‘unga’ (kipara)
na kwamba wakati wa Tanzania kuongozwa na vijana
haujafika.
Ingawa Mokiwa hakutaja moja kwa moja jina la January,
lakini ndiye kijana pekee ambaye ametangaza nia ya
kuwania urais na kudai ni wakati wa vijana kushika
hatamu za uongozi.
Wasomi nao wamshauri
Baadhi ya wasomi nchini wamemtaka January kufuata
ushauri aliopewa na Rais Jakaya Kikwete, asilazimishe
kuwania nafasi ya urais kwa sababu wakati ukifika
atapata. Akiichambua kauli hiyo, Mhadhiri wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Benson Bana,
alisema haiwezekani kwa mtu kupewa nafasi ya uongozi
kama hana uzoefu wa kazi. Dk. Bana alisema kutokana
na hali hiyo ndio maana hata, Rais Kikwete

mzee makamba
 alitengenezewa njia kabla ya kupewa jukumu la
kuiongoza nchi. Mhadhiri mwingine wa UDSM, Profesa
Hajji Semboja alisema kauli ya Kikwete ni ya kiongozi
mwenye hekima na busara. Alisema kila chama kina
utaratibu wake wa kuchagua wagombea, hivyo alipaswa
kufuata utaratibu huo kabla ya kutangaza hadharani.
Kauli ya Kikwete imekuja siku chache baada ya January
kutangaza kuwania nafasi hiyo wakati akihojiwa na
Shirika la Habari la Uingereza (BBC), wiki iliyopita.

No comments: