![]() |
Justin Bieber |
Mwimbaji kutoka Canada, Justin Bieber hatimaye amepewa haki
yake kufuatia kosa alilolifanya la kurusha mayai zaidi ya 20 kwa jirani
yake na kusababisha hasara ya uharibifu wa ukuta na mali.
Akiwakilishwa na wakili wake, Shawn Holley mahakamani hapo, Justin Bieber amehukumiwa kufanya kazi za jamii (usafi wa mazingira) kwa muda wa siku tano na kulipa fidia ya $80,900 kwa uharibifu alioufanya.
Hukumu hiyo inamuamrisha Bieber kukaa umbali usiopungua hatua 100 kutoka kwa jirani yake na familia ya jirani huyo kwa muda wa miaka miwili, na kuhudhuria matibabu ya kudhibiti hasira.
Hata hivyo ni rahisi sasa kwa Justin Bieber kukaa umbali huo na jirani yake kwa kuwa ameshahama katika maeneo aliyokuwa anaishi zamani na sio jirani wa mlalamikaji tena.

No comments:
Post a Comment