![]() |
| Kiongozi wa Muslim Brotherhood Mohammed Badie [katikati[ |
Mahakama moja nchini Misri imemhukumu kifungo cha
maisha jela kiongozi wa kundi la Muslim Brotherhood Mohammed Badie na
wanachama wengine 36.
Watu hao walipewa hukumu hiyo kwa kuchochea
ghasia na kufunga barabara wakati wa maandamano baada ya jeshi kumpindua
aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi mwaka uliopita.Bwana Badie tayari anakabiliwa na hukumu nyengine ya kifo kutoka kesi nyingine.
Mahakama hiyo ya mjini Cairo pia iliwahukumu vifo wanachama wengine kumi wa kundi la Muslim brotherhood.
Makundi ya haki za kibinaadamu yamekosoa misururu ya hukumu za kifo nchini Misri yakisema zilishinikizwa kisiasa.

No comments:
Post a Comment