 |
Linah & David Banner |
Linah amepata nafasi ya kufanya kazi na rapper ambaye pia ni
mtayarishaji mkubwa wa muziki na mshindi wa Grammy kutoka Marekani,
David Banner.
David Banner na Linah walikutana studio na watayarishaji wengine
akiwemo P-Funk Majani, Lamar, Nahreel na Ematheboy na kwa pamoja
watayarishaji hao walitengeneza mdundo.
Akiongea na Bongo5, Lamar ameeleza baada ya kufanya mdundo David
Banner aliingiza sauti na baadae Linah akaweka chorus na imebaki verse.
 |
Pichani,Kushoto ni Lamar,David Banner,Nahreel,Ema the Boy & PFunk Majani. |
“Sisi tulikutana tu tukaanza kutengeneza beats, tumekata samples pale
tukaanza kushauriana tufanye vipi, halafu akaingiza sauti David Banner
kama chance tu na Linah akaingiza chorus ikawa bado kuingiza verse,
yaani tulikuwa tunafanya vitu kwa pamoja, tunatengeneza beat kwa pamoja.
Project ambayo amefanya Linah na David Banner itaendelea tunafinalize.”
Amesema Lamar..
No comments:
Post a Comment