Mch,JOSEPHAT GWAJIMA |
Habari toka chanzo cha kuaminika kilichopo ndani ya kanisa la mchungaji
huyo ni kuwa Gwajima hivi sasa ameshauza karibia robo tatu ya mali zake
na kwamba moja kati ya magari yake ya kifahari huenda likanunuliwa na
mwanamuziki Diamond.
“Jamaa hivi tunavyoongea anaweza akawa ameshatoroka tayari, maana hili
sakata limeanza kumwendea hovyo na wiki iliyopita kuna madalali walikuja
hapa wakiitaka gari yake aina ya Hammer, wakidai kuwa inataka
kununuliwa na mwanamuziki Diamond,” kilisema chanzo cha habari hii.
Kikaendelea kumwaga data kuwa karibu wiki zima lililopita mchungaji huyo
alikuwa kwenye mipango ya kuuza baadhi ya nyumba zake na kwamba hata
familia yake hivi sasa haiko kwenye makazi yake anayoishi siku zote…
“Hata familia yake sijaiona karibu wiki mbili hapa kanisani na taarifa
tulizonazo karibu waumini wengi tu ni kwamba jamaa anataka kuhama nchi
lakini hatujui ni nchi gani anayotaka kwenda kufanya makazi yake tena ya
kudumu,” alisema.
Habari hizo zinadai kuwa baadhi ya waumini wamepanga kugawana mali
kadhaa za kanisa pamoja na za Gwajima mwenyewe endapo itagundulika kuwa
ametoroka kweli….
Flora Mbasha |
“Kuna baadhi ya waumini wamekerwa sana na hii skendo ya Flora Mbasha,
wamekuwa wakijiapiza kwamba hata zile mali zake ni halali yao kwani
zinatokana na sadaka wanazotoa kila siku, inasikitisha sana kwa kweli.”
alisema mtoa habari hii.
Inasemekana kuwa mchungaji Gwajima amepanga kuwaaga waumini wake kama
vile anakwenda kueneza neno katika mataifa mengine, lakini ukweli ni
kwamba anataka kuondoka ili kukwepa aibu kutokana na mambo
yanayoendelea…
Flora Mbasha & Mumewe Emmanuel Mbasha. |
“Jamaa yupo kwenye hali ngumu, hii ishu ya Flora Mbasha imemuweka katika
wakati mgumu sana kwa sababu amekuwa akinyooshewa vidole sana, na kuna
baadhi ya wazee wamekuwa wakimtaka atoe tamko rasmi ili kukwepa hiki
kikombe cha aibu,” kilisema chanzo hicho.
Mwandishi alimpigia simu Gwajima lakini simu yake haikupatikana, na hata
Diamond naye alipopigiwa simu ili kujua kama kweli anataka kununua gari
la Gwajima, simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe
mfupi hakujibu kitu
No comments:
Post a Comment