Wednesday, 9 July 2014

ROSE MUHANDO AELEZA TAMANIO LAKE KWA UWEPO WA ANASTAZIA MUKABWA KWENYE UZINDUZI WA ALBAM YAKE MPYA.

Anastazia Mukabwa & Rose Muhando.
Mwimbaji nguli wa muziki wa Injili nchini Kenya, Anastazia Mukabwa, ni miongoni mwa wakali ambao mwimbaji Rose Muhando anatamani wawepo kwenye uzinduzi wa albamu yake ya Kamata Pindo la Yesu. Rose Muhando amepanga kuzindua albamu yake ya Kamata Pendo la Yesu Agosti 3, mwaka huu Kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Inadaiwa kuwa Mukabwa ni aina ya wasanii wenye uwezo mkubwa wa kuimba na kwamba Rose ameiomba Kamati ya Maandalizi ya uzinduzi wake iwasiliane na msanii huyo mapema kuhakikisha anapatikana siku hiyo. “Wapo waimbaji wengi wa Injili natamani wawepo siku hiyo, lakini ningefurahi sana  kama ningempata Anastazia Mukabwa wa Kenya, hivyo tayari nimeiomba Kamati yangu ya Maandalizi ifanye kila linalo wezekana aje, Nyimbo zilizopo katika albamu ya Kamata Pindo la Yesu ni Bwana Niongoze, Wewe Waweza, Usiniache, Nibariki, Muongo, Kwema, Kamata Pindo la Yesu na Facebook inayofanya vizuri zaidi.
Ikumbukwe kuwa Anastazia Mukabwa na Rose Muhando walishawahi kukutana kwenye Albam ya pamoja iliyofanya vizuri sana kwenye ukanda huu wa Africa Ya Mashariki hapo Awali,Albam waliyoipa jina la KIATU KIVUE,huku wimbo wa KIATU KIVUE ukikaa kwenye Chati nyingi za muziki wa Injili Africa ya Mashariki.

No comments: