Vyombo
vya habari nchini Brazil vimeripoti kuwa Meneja wa Timu ya Taifa hilo Luiz Filipe Scolari amejiuzulu
rasmi nafasi yake hiyo ya umeneja wa timu ya taifa. Tangazo rasmi linatarajiwa
kutolewa baadaye (leo). Scolari ambaye analaumiwa kwa kuisababishia timu hiyo ya Taifa{Brazil}kichapo
cha mabao 7-1 na Ujerumani alishasema awali kuwa nafasi yake hiyo
itafikiriwa upya na chama cha soka cha Brazil baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia.

No comments:
Post a Comment