Monday, 21 July 2014

Viungo vya binadamu (idadi kubwa) vyaokotwa Bunju-Machimbo

UPDATES:-
Idadi hiyo imeokotwa ktk mifuko ya viroba......ni hali ya kusikitisha kwa kweli miongoni mwao wapo watoto.
**Kwa mujibu wa Radio One:
Jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni limesema kuwa limekamata viungo mbalimbali vya binadamu vilivyohifadhiwa ktk mifuko ya plastiki ktk machimbo ya kokoto ya Bunju nje kidogo ya jiji la Dsm
***TBC wametangaza sasa hivi kuwa ni viungo vya binadamu ambavyo vilikuwa kwenye mifuko vimekutwa katika eneo la kutupia takataka lakini idadi haijasemwa kwakua imefika kama habari iliyofika punde (breaking news) kwahiyo bado hawajotoa taarifa kiundani.
***Hii habari imetangazwa sasa hivi na ITV. Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi.
*** Idadi hiyo imeokotwa ktk mifuko ya viroba......ni hali ya kusikitisha kwa kweli miongoni mwao wapo watoto.
***HABARI HII BADO HAIJATHIBITISHWA KWA MAPANA NA JESHI LA POLISI***

No comments: