Monday, 21 July 2014

VJ Penny abadili kidole cha pete yake, Je amechumbiwa au ni Mbwembwe!?

Vj Penny
VJ Penny aliyekuwa mchumba wa Diamond Platinumz amepost picha inayoonesha kwa ukaribu akiwa na pete kwenye kidole cha pete, picha iliyozua hisia nyingi kuwa amechumbiwa ama la.. kwa kuwa hakuipa maelezo.
“Road trip ….site her we come…cc @halimakimwana1.” Aliandika Penny.
Kidole chenye pete mkononi mwa Vj Penny
Ingawa watu wengi walioamini kuwa VJ Penny amechumbiwa walimpa honger zake kwenye Instagram bado kuna walakini kwa kuwa siku 6 zilizopita alikuwa amevaa pete hiyo hiyo.
Je, amechumbiwa kweli au amehamishia pete hiyo kwenye kidole kingine kwa swag!?
Wakati bado unatafakari jibu ambalo bila shaka yeye binafsi ndiye anaeujua ukweli wa mambo, naomba nikuunganishe na hisia nyingine zitakazolisogeza jibu lako karibu na ukweli au kukutoa kwenye ukweli.
VJ Penny ambaye kwa mujibu wa ‘words on the street’ inadaiwa alikuwa chaguo la kwanza la mama Diamond Platinumz ameweka picha hiyo siku moja baada ya Wema Sepetu kupost picha nyingi kwenye Instagram akiwa na mama Diamond kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa na kuzipa caption mbalimbali huku nyingine zikiwa na vijembe.
Hata hivyo, mwaka jana VJ Penny aliongea na Bongo5 kuhusu uhusiano wake na Diamond na kueleza kuwa yale yalikwisha na amejipanga kufanya mambo yake huku akiamini kuna mtu mwingine atakayestahili nafasi kwake.
Tunampa hongera zote VJ Penny kama ni kweli amechumbiwa, lakini kama ni swag tunampa hongera pia because she looks good kama kawaida yake.

No comments: