Monday, 11 August 2014

KUNDI LA ORIGINAL KOMEDI LAVUNJIKA.....

Hakuna ubishi kuwa miaka michache iliyopita kundi la Orijino Komedi ndilo kundi lenye mashabiki wengi hapa nchini. Ilikua ikifika muda wa kurushwa kipindi kila mtu alikuwa hang'oki Katika TV yake. Umaarufu  wao uliongezeka zaidi pale walipohama EATV na kuhamia TBC.
Umaarufu wao uliendelea kuwepo hadi siku za karibuni ambapo ulishuka kwa kasi sana, taarifa ambazo Bongoclan imezipata ni kuwa kwa sasa kundi  hilo limevunjika na kila mtu anafanya kazi kivyake. Chanzo chetu kutoka kituo cha TV walichokua wakifanya kazi kiasema kuwa kwa sasa kila mtu ana hamsini zake na hawafanyi kazi tena pamoja

No comments: