Thursday, 28 August 2014

LUPITA NYONG'O NA KNAAN SASA NI LIVE BILA CHENGA.

Lupita Nyong'o & Knaan

WASANII maarufu kutoka Afrika wanaotamba katika ngazi za kimataifa -- K’Naan kutoka Somalia aliyetamba sana na wimbo wake wa Kombe la Dunia mwaka 2010 na mwanadada wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kushinda Tuzo za Oscar, Lupita Nyong’o, wameonekana wakiwa pamoja katika mgahawa mmoja huko Brooklyn, Marekani.
Wapenzi hawa walihisiwa kuwa wana uhusiano wa kimapenzi tokea mwezi wa tisa mwaka jana, ila walikuwa wakijificha sana na hatimaye juzi kubambwa live wakishikana mikono na mabusu teletele hadharani.

Wakali hawa wanaoiwakilisha Afrika vizuri hawana sababu tena ya kuficha mapenzi yao, hivyo wengine tubaki kulia na kuwapa sapoti zote watakazohitaji kwani kazi zao zinakubalika.

No comments: