PICHA-Rapa bora wa kike, Onika Tanya Maraj 'Nicki Minaj' akiwa katika pozi tata na Aubrey Drake Graham 'Drake' wakiwa katika utengenezaji wa video ya wimbo Mpya wake Nicki Minaj‘Anaconda’.
Nicki Minaj anaendelea kuvuta umakini wa watu kuisubiria kwa hamu video ya wimbo wake Mpya‘Anaconda’ ikiwa ni siku kadhaa baada ya kutoa kipande cha video kinachoonyesha utengenezwaji wake. Jana August 18, 2014 Nicki ameshare tena picha nyingine za video hiyo inayomuonesha yeye akiwa amekaa katika mtindo wa kimitego tata mbele ya mwenzie toka Lebo ya YMCMB Drake aliyekaa kwenye kiti. Anaconda ni wimbo mpya unaotoka kwenye albam ya ‘The Pink Print’ ya rapper huyo wa Young Money,Nicki Minaj anatarajiwa kuuimba wimbo huo Live wakati wa utoaji wa tuzo za MTV Video Music Awards, Jumapili, August 24.



No comments:
Post a Comment