Saturday, 30 August 2014

Ray na Ostaz Juma si wapenzi wangu-Johari

Johari-Kikaangoni Live{EATV}
Mwanadada anayefahamika kama Blandina Chagula (Johari) amefunguka na kuweka wazi kuwa hajawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Muigizaji mwenzake Ray
wala Ostaz Juma kama ambavyo imekuwa ikizushwa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari,Johari amefunguka hayo kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV wakati akichat Live katika kipengele cha Kikaangoni Live. "Ni kweli haya mambo yanakuwa yanatokea na kuzushwa lakini ukweli kwamba sijawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Ray lakini mahusiano yetu ni ya kikazi tu,lakini pia sijawahi kuwa na uhusiano na Ostaz Juma" Mwanadada huyo ambaye alijipatia umaarufu kwa kuweza kuuvaa uhalisia katika Movie anazokuwa akifanya amesema kuwa amekuwa kimyaa katika Tasnia ya filamu kwa kuwa alikuwa akijipanga ili kuleta mabadiliko katika tasnia hiyo,mbali na hilo Johari alieleza sababu ya Filamu nyingi za kitanzania kuonekana kufanana na kusema kuwa hiyo inasababishwa na maisha ya bara letu la kiafrika kuwa na matatizo yanayofanana katika kila familia na kila ngazi. "Filamu zetu zinaonekana kufanana kwa namna moja au nyingine kutokana na ukweli kwamba maisha ya waafrika na matatizo yao yanafanana hivyo hupelekea kuleta mfanano katika kazi ingawa lazima kutakuwa na tofauti kidogo " BIFU Mwanadada Johari ameweka wazi kuwa hajagombana na baadhi ya wasaniii wenzake kama ambavyo imekuwa ikinukuripotiwa na baadhi ya watu kuwa amegombana na Chuchu na kupigana na Mainda kisa ni kugombea mwanaume ambae alitwajwa kuwa ni Ray. "Ni kweli Ray ni mkurugenzi mwenzangu katika kampuni yetu RJ ila sina mahusiano nae kimapenzi na sijawahi kugombana na chuchu wala msanii mwingine yoyote yule kwa sababu ya mahusiano ya mapenzi" USHAURI WAKE KWA WASANII WACHANGA Siku zote ukubwa jalala hivyo mwanadada Johari anaonesha ukomavu wake katka tasnia kwa kuwachana baadhi ya wasanii wanaochipukia katika tasni ya filamu na kuwataka kuitunza tasnia na kuhakikisha wanaikuza kama ambavyo wao walifanya miaka kadhaa iliyopita. "Kiukweli nawashauri wasanii wachanga hata wale ambao teyari ni wakongwe waache kuchafua tasnia maana kama sisi tungeiharibu mwanzo sidhani kama wao wangeweza kufika hapo walipo hivyo waitunze tasnia ili hata vizazi vijavyo viikute na kuindeleza kama ambavyo sisi tuliweza kufanya hivyo"

No comments: