![]() |
| Steve Nyerere |
Muigizaji aliyepata umaarufu zaidi kwa kuigiza sauti ya mwalimu Nyerere, Steve Nyerere ametangaza nia yake ya kutaka kugombea ubunge mwaka 2015 katika jimbo la Kinondoni. Muigizaji huyo ambaye ni mwenyekiti wa Bongo Movie Unity ameiambia Bongo5 kuwa tayari amejipanga kuwania kiti hicho kwa tiketi ya CCM. “Ukiona chereko chereko ujue mambo yameiva, yeah nitagombea ubunge mwakani. Nimejipanga na ninaweza kufanya hivyo, nipo vizuri sana.” Amesema Steve Nyerere.
Source: Bongo5

No comments:
Post a Comment